Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.
MASHINDANO ya Njalu Cup yaliyoshirikisha timu 20 Kutoka Jimbo la Itilima, yamefikia ngazi ya Fainali Kwa kuzikutanisha timu za Langangabili Fc na Mwamtani Fc.
Mashindano hayo ambayo yanadhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silanga, yameibua vipaji kwa Vijana pia yamekutanisha wadau wa michezo.
Katika mashindano hayo kila timu iliyoshiriki itakabidhiwa kiasi cha shilingi 100,000 ambapo Mshindi wa nne atapewa kaisi cha shilingi 500,000, Mshindi wa tatu atapewa shilingi Mil.1, Mshindi wa pili Mil. 2 na Medali, na Mshindi wa kwanza atapewa shilingi Mil. mil.3, Kombe na Medali.
Mwisho.







0 Comments