KULINGANA na Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bei ya mafuta ya petroli imepanda kwa kiwango kikubwa ambapo kwa Jiji la Dar es Salaam imepanda toka shilingi 2,864 kwa lita mwezi Machi hadi kufikia shilingi 3,820 kwa lita mwezi Aprili 2026.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa kupanda kwa bei kunatokana na mabadiliko ya soko la kimataifa, likiwemo ongezeko la bei ya mafuta ghafi na changamoto za usafirishaji. Aidha, hali ya kisiasa na kiusalama duniani, hususan mvutano unaoendelea kati ya mataifa mbalimbali, imechangia kuvuruga upatikanaji na usambazaji wa mafuta katika masoko ya kimataifa.
Kwa mujibu wa EWURA, gharama za uagizaji na usafirishaji zimeongezeka, zikichangiwa pia na kupanda kwa gharama za bima ya meli pamoja na ucheleweshaji wa mizigo. Hali hii imepelekea bei za rejareja kupanda katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, ambako bei mpya zimeanza kutumika rasmi kuanzia leo Aprili Mosi mwaka huu.
Kutokana na ongezeko hilo, wananchi wametakiwa kutumia nishati kwa uangalifu na kuzingatia mbinu mbadala ili kupunguza gharama. Serikali kupitia EWURA imeeleza kuwa itaendelea kufuatilia mwenendo wa bei za mafuta duniani na kuchukua hatua stahiki kulinda maslahi ya watumiaji wa ndani.






0 Comments