NA Berensichina Meatu
JUMUIYA ya hifadhi ya Wanyamapori Makao wilayani Meatu mkoani Simiyu imewakatia bima za afya wazee 100 kutoka katika vijiji 9 vinavyounda jumuiya hiyo ambapo sasa wazee hao wataweza kutibiwa bure kwa kipindi cha mwaka mzima katika hosptal .
Akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi bima hizo iliyofanyika mjini Meatu mwenyekiti wa jumuiya hiyo Daniel sengela amesema wameamua kutoa bima hizo kwa wazee hao ikiwa ni mpango wao baada ya kuona wazee hao walivyokuwa wakisumbuka kupata matibabu pindi wanapougua.
"Tuliona ni vema tuwasaidie wazee hao ambao ni wanachama wa jumuiya yetu ili wasisumbuke kupata matibabu ambapo pia tutaendelea kuwasaidia kwa mambo mengine pia kadili ya uwezo wetu."alisema mkiti huyo.
Kwa upande wao wazee hao waliopatiwa bima hizo hawakusita kuonyesha furaha yao ambapo wameupongeza uongozi wa jumuiya hiyo kwa kuwajali katika suala la afya na sasa wameondokana na adha ya kupata huduma ya afya.
Maduhu ngudungu kutoka kijiji cha iramba ndogo amesema kwao wanaona kama miujiza kwa kupewa bima hizo kwani ni muda mrefu sasa wamehangaika na matibabu.
Mwisho


0 Comments