
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imewaonya watoa huduma ya usafirishaji wasitumie ongezeko la bei za mafuta kuwaumiza wananchi kwa kupandisha nauli kiholela.
Mkurugenzi Mkuu, Habibu Suluo, amesema leo kuwa hiki ni kipindi cha mpito na watoa huduma wanapaswa kushirikiana badala ya kuchukua hatua peke yao.
"Ninawaomba wasafirishaji, msitumie nafasi hii kuwaumiza Watanzania. Tukiwabaini watakaofanya hivyo, tutachukulia hatua kali," alisema Suluo.
LATRA imeitisha kikao cha dharura kwa watoa huduma cha Aprili 8, kitakachorushwa mubashara kwenye vyombo vya habari, ili wananchi na wadau mbali pia waweze kutoa maoni yao.
Suluo alisisitiza: "Usiachie wananchi kubeba mzigo huu peke yao. Kaa kwenye meza ya mazungumzo kwanza – ushirikiano ndiyo suluhisho."
Watoa huduma wanahimizwa kushirikiana na LATRA ili kupitia kipindi hiki cha mpito bila kuumiza wananchi.
Mwisho.
0 Comments