NYAROBI M. LUGATA ALAMBA UTEUZI SKAUTI-SIMIYU

 

Nyarobi Mabula Lugata (Dj Nyaro).


Na Sakagoi Kapagala, Bariadi.


CHAMA Cha Skauti Mkoa wa Simiyu, kimemteua Nyarobi Mabula Lugata (Dj Nyaro), kuwa Mkuu wa Idara na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Skauti Mkoa wa Simiyu kuanzia January 2026.



Katika barua ya Uteuzi yenye KUMB Na.RSC/SMY/RXC/3, iliyotolewa na Kamishna wa Skauti Mkoa wa Simiyu, Insp.Francis Msuku imeeleza kuwa kutokana na kuongeza uhitaji na kuboresha jitihada za kuendeleza Skauti Mkoa wa Simiyu, Kwa niaba ya Bodi ya Skauti Mkoa, na kwa mujibu wa katiba ya Chama cha Skauti Tanzania Ibara ya 9 na POR. Ibara ya 101-105.1 uk 79-83.


Taarifa hiyo imefafanua, kwa mujibu wa sera ya watu wazima na mafunzo ya Taifa ya mwaka 2016, kuanzia tarehe 30/1/2026, ameteuliwa rasmi kuwa "MRATIBU MKUU IDARA YA UTAWALA BORA, UWAJIBIKAJI NA MIKAKATI MKOA WA SIMIYU." 


Mwisho.




Post a Comment

0 Comments