MKUU wa Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu, Simon Simalenga (kushoto) akipewa maelezo na Mkaguzi wa Pamba wilaya hiyo, Ndinda Anthony namna wadudu wanavyoshambuliwa Pamba.Na Mwandishi wetu, Bariadi.
MKUU wa Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu, Simon Simalenga ametembelea na kukagua mashamba ya zao la Pamba yaliyopo Mwakibuga kata ya Nyakabindi pamoja na kijiji cha mwamondi ili kujionea Maendeleo ya zao hilo pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wakulima.
MKUU wa Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu, Simon Simalenga (kushoto) akipewa maelezo na Mkaguzi wa Pamba wilaya hiyo, Ndinda Anthony namna ya kudhibiti wadudu wanavyoshambuliwa Pamba.Simalenga, amezisisitiza Kampuni za Pamba hususani zilizowekeza katika Kilimo Cha pamba kuzingatia utaratibu na makubaliano ya kupeleka fedha kwa wakati na kwamba serikali haitasita kuwachukukulia hatua.
"Niwape Rai, na angalizo mapema kwamba ikitokea Kampuni imewekeza kwenye kata fulani halafu msimu wa mavuno mwananchi akapeleka Pamba na mwenye Kampuni hapeleki fedha, safari hii wajipange kabisa..., tutapeleka mnunuzi mwingine" amesisitiza Simalenga.
Mwisho.





0 Comments