Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, CP Salum Hamduni (kulia), akizungumza na Viongozi kutoka Mkoa wa Simiyu waliokwenda kujifunza masuala ya Usafi wa Mazingira.Na COSTANTINE MATHIAS, Shinyanga.
MKOA wa Shinyanga, umepokea ujumbe wa Viongozi kutoka Halmashauri za Itilima, Busega na Bariadi mkoani Simiyu waliowasili kwa ajili ya kujifunza mbinu bora za usafi wa mazingira na utunzaji wa Mazingira.
Imeelezwa kuwa kwa miaka mitatu mfululizo, Manispaa ya Shinyanga imeendelea kuwa kinara wa usafi wa mazingira nchini, mafanikio ambayo yanavutia Halmashauri mbalimbali kwenda kujifunza ili kuboresha maeneo yao.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, CP Salum Hamduni, amepokea na kuukaribisha ujumbe wa Viongozi hao na kuwatakia mafunzo yenye mafanikio, huku akisisitiza umuhimu wa kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika kuimarisha usafi na afya za wananchi.
Mwisho.







0 Comments