LAGANGABILILI FC, WATWAA KOMBE LA NJALU-ITILIMA. ‎

Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.

‎TIMU ya Langangabili Fc imetwaa kombe la Njalu kwa kuwafunga Mwamtani Fc Magoli 3-0, michezo wa fainali ambao umefanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Langangabili.

‎Katika fainali hiyo ambayo ilitanguliwa na mchezo wa Kutafuta Mshindi wa tatu kati ya  Chinamili na Nkuyu ambapo mchezo huo ulitamatika kwa Chinamili Fc kuwafunga Nkuyu Fc goli 1-0.


‎Joel Makwaiya, Katibu wa CCM Itilima, amesema Mbunge wa Jimboa Itilima, Njalu Silanga ameandaa Utaratibu wa kukutanisha vijana kupitia michezo na kwamba amekuwa akitoa fedha za kudhamini mashindano ya Njalu cup.

‎"Mashindano haya tunatafanya sababu nchi Ina amani, wananchi muendelee KUMUUNGA mkono Rais Samia, ili tuendelee na michezo" amesema Makwaiya.

‎Mbunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga amewapongeza Wana michezo kwa kushiriki mashindano hayo pamoja na waamuzi ambao wamesimamia kuhakikisha yanatamatika.

‎"kazi kubwa mmesimamia mpaka mashindano haya yakafanyika, nizipongeze timu zote zilizoshiriki, michezo ni ajira, sehemu ya kufahamiana na kujiendeleza, Leo Kuna fahari kubwa ya Njalu Cup" amesema na kuongeza.

‎"Mashindano hayo ya Njalu cup ulianza 2012, nilisema 2023, lazima tubadilishe kombe na tumefanikiwa kuleta kombe jipya...vijana Leo tunahitimisha michezo, waratibu wataratibu ili washindane liwe la kwao moja Kwa moja"

‎Njalu amesema kuwa pamoja na kushiriki  michezo, lazima vijana wajisughulishe na shughuli za Maendeleo ili wawe na vipato vya halali ambapo aliwaasa vinana pamoja na walezi kufundisha nidhamu na amani katika kizazi hiki.


‎"Elimu iwe sehemu ya kujipatia kipato na siyo kuvuruga amani, vijana mkitulia na nchi itatulia, Wana michezo muwe mabalozi wa kuzungumzia amani, vijana kuweni walinzi wa familia na Itilima yetu ili tulete Maendeleo." Amesema Njalu.

‎Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Ana Gidarya amesema kuwa Michezo ni kutekeleza ilani ya CCM huku akizipongeza Kamati za uratibu pamoja na washiriki walifanikisha mashindano hayo.

‎"Tutunze amani ya nchi yetu, na kulinda Kwa wivu Mkubwa, na vijana mnaendelea kufanya shughuli zenu za kujipatia kipato, hakuna Tanzania nyingine, Tanzani ni moja tu" amesmaa.

Katika mashindano hayo kila timu iliyoshiriki itakabidhiwa kiasi cha shilingi 100,000 ambapo Mshindi wa nne atapewa kaisi cha shilingi 500,000, Mshindi wa tatu atapewa shilingi Mil.1, Mshindi wa pili Mil. 2 na Medali, na Mshindi wa kwanza atapewa shilingi Mil. mil.3, Kombe na Medali. 

‎Mwisho.








Post a Comment

0 Comments