Na Mwandishi wetu.
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Mji Bariadi limefanya mkutano leo, tarehe 13 Agosti 2026, kwa lengo la kujadili utekelezaji wa shughuli za Halmashauri katika kila kata kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Bariadi, ambapo madiwani wamepata fursa ya kupitia na kujadili kwa kina utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa katika kata za Halmashauri hiyo.
Majadiliano hayo yamelenga kutathmini hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mipango na miradi ya Serikali, kubaini changamoto zilizojitokeza pamoja na kuweka mikakati ya kuhakikisha shughuli za maendeleo zinakamilika kwa wakati na zinawanufaisha wananchi.
Mkutano huo umehudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani,Watendaji wa Kata pamoja na Wakuu wa Idara na vitengo na Idara kutoka Halmashauri ya Mji Bariadi.
Mwisho.














0 Comments