Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge akiuliza swali Bungeni leo Juni 10, 2026.
Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.
SERIKALI kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekeza nguvu kubwa kulinda Uvuvi wa asili ambao ni chanzo kikubwa cha mazao ya samaki kuliko Uvuvi Mbadala na kwamba serikali imejipanga kuleta sheria Bungeni ili kuunda Mamlaka ya Uvuvi ambacho ni chombo madhubuti kuweza kusimamia rasilimali za Uvuvi.
Haya yamebainishwa leo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dk. Bashiru Kakurwa, wakati akijibu swali na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge aliyetaka kujua kuhusu Mkakati wa Serikali kuhusu Upungufu wa samaki Ziwa Viktoria na uzalishaji wa vifaranga katika Ziwa Victoria.
Tina Chenge aliuliza "Kwa Sasa hivi Kuna upungufu Mkubwa samaki katika Ziwa Viktoria, Je serikali haioni umuhimu wa kuja na Sheria ua mwongozo utakaoruhusu vifaranga vya samaki kuzalishwa kwenye vizimba baadae vikarudishwa Ziwani ili viendelee kukua na kuzaliana sambamba na kutenga maeneo Maalumu Kwa ajili ya breeding ambapo hakutaruhusiwa kuwa na Uvuvi wa aina yoyote Ile?."
Waziri Balozi Dk. Kakurwa amesema "Ndio Mwelekeo ambao tutakuwa nao kama nilivyosema hili ni eneo jipya linatusaidia kusema Ukweli kuongeza uzalishaji wa samaki Kwa sababu Uvuvi wa asili samaki wameanza kupungua na Kwa kiwango kikubwa ni kutozingatia Uvuvi usiofauata Sheria Kwa hiyo inabidi tufanye kazi mchanganyiko (Mbinu mchanganyiko)," amesema na kuongeza.
"kwanza ufugaji wa samaki wa vizimba si mbadala wa Uvuvi wa asili,.lazima tuwekeze nguvu kubwa sana kulinda Uvuvi wa asili sababu ndio chanzo kikubwa Cha mazao ya samaki kuliko huu Uvuvi ambao ni mbadala na Kwa maana hiyo serikali imejipanga kuleta Sheria hapa Bungeni ili kuunda chombo madhubuti, Mamlaka ya uvuvi kuweza kusimamia rasilimali za Uvuvi ili tuongeze rasilimali na tuzilinde la pili ni kaunza kufanya re stocking ya kutengeneza vifaranga na kuvipandikiza halafu na kutenga maeneo yaliyohofadhiwa na kuongeza uzalishaji wa samaki."
mwisho.
![]() |





0 Comments