MSEMAJI wa Timu ya Simba, Ahmed Ally amekutana na Mashabiki wa Simba mjini Bariadi Mkoani Simiyu wakati akipita kuwasaalima alipokuwa akitokea kwenye Uzinduzi wa Mashindano ya Goyayi cup Kijiji cha Sawida wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.
Msemaji huyo alipita kusalimiana na Mashabiki wa Simba wakati akielekea jijini Mwanza kupanda ndege kurudi Dar es salaam kuendelea na majukumu yake.
Katika ujumbe wake kwa Wanasimba, Msemaji huyo ameeleza furaha yake kufika Bariadi kwani siyo mara ya kwanza bali amefika mara kadhaa na akiwa Msemaji wa Simba hi ni mara ya kwanza.
"Nimefurahi kuona watu wengi wamevaa jezi za msimu huu, hongereni sana Wana Bariadi kuiunga mkono Simba ni pamoja na kununua bidhaa original za klabu yetu ndipo Mzabuni anapata nguvu na faida ya kutimiza malengo na ahadi alizotuahidi... Nyote mnaona wiki hii hadi inakwemisha ametimiza ahadi yake kubwa ya kutununulia basi jipya la kisasa aina ya Irza, tayari limeshafika," amesema na kuongeza.
"Busi hiyo linafanyiwa Branding tayari linaingia mtaani, ahadi hizi ambazo anazitoa zinatimia na sisi Wanasimba ni wa kutimiza hizo ahadi, tunatimizajie? Ni kununua jezi original, niwasifu kweli hapa Bariadi sijaona mtu amevaa jezi feki, tujiandae na jezi mpya msimu ujao"
Mwisho.










0 Comments