AHMED ALLY AZINDUA MASHINDANO YA GOYAYI CUP SAWIDA-ITILIMA.



‎Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.

‎MSEMAJI wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amezindua mashindano ya Goyayi CUP yaliyoanza kufanyika jana Juni 5, 2016 katika Kijiji cha Sawida wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu yenye lengo la kukuza vipaji kwa Vijana na kuendeleza soka la Mkoa wa Simiyu na Taifa kwa ujumla.

‎Akizungumza jana kabla ya kuzindua mashindano hayo ambayo yatahusisha timu 22 kutoka wilaya ya Itilima, Kwimba na Magu, Msemaji huyo amesema Mwanzilishi Mashindano hayo (Peter Goyayi) anapaswa kuungwa mkono ili aendeelee kuwafanyia mema wana michezo hasa wakazi wa Sawida kwani amelenga kuwaunganisha kupitia michezo.

‎"Nimefurahi kufika Sawida na kukutana na wanasimba na wapenda michezo, nimeona kuna mwamko Mkubwa wa mchezo hasa mpira wa miguu, tumuunge mkono Mwanzilishi wa mashindano haya ambaye amewafanya vijana kuonekana kupitia vipaji vyao vya mpira" amesema.


‎MSEMAJI wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally akizungumza wakati wa kuzindua mashindano ya Goyayi CUP yaliyoanza kutimua mvumbi katika Kijiji cha Sawida wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.

‎Amewataka waandaaji wa Mashindano kama hayo kuyaandaa kwa malengo kuliko kusubiri muda wa kuomba kura ili kuwasaidia vijana kwenye mpira wa miguu, huku akisisitiza kualika watu wenye maamuzi ili wafanye usajili wa vijana kutoka maeneo mbalimbali pi kushirikisha wataalamu ambao wamesomea mpira ili waweze kupata wachezaji kutoka ngazi ya chini.

‎Akisoma taarifa ya mashindano hayo Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Goyayi Cup, Kelvin Peter, amesema Lengo la Mashindano hayo ni kurudisha fadhila Kwa jamii, ambayo imekuwa ikiwaunga mkono katika shughuli zao kibiashara.

‎"Tunaanda mashindano haya kwa lengo la kugundua vipaji, timu zimejiandaa kutoa burudani, kutakuwa na motisha, kombe, jezi na zawadi kwa wachezaji... changamoto kubwa huku ni Uhaba wa Miundombinu ya michezo, tunaomba ofisi ya Diwani kutenga muda wa kushiriki na kulinda maeneo ya michezo.


‎Mkurugenzi ww Goyayi cup, Peter Goyayi akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa uzinywa mashindano hayo yaliyoanza kurindima katika uwanjia wa shule ya Msingi Sawida.

‎Amemtaka Msemaji wa Simba, Ahmed Ally kuunga mkono mashindano hao huku wakimwomba kuwa balozi wa Mashindano hayo pamoja na kufikisha ujumbe, kwani watamani kuona siku moja wachezaji wa goyayi CUP wakicheza ligi Kuu.

‎kwa Upande wake Mkurugenzi ww Goyayi cup, Peter Goyayi amesema lengo la mashindano hayo ni kukuza vipaji vya vijana ambao wanateketea kwa ulevi bila kuwa na Mwendelezo.

‎"Lengo ni kukuza vipaji vya michezo kwa vijana wengi wanaopoteza matumaini katika soka, tumelenga Kusaidia kukuza soka la Mkoa ambalo halina hata kiwanja cha michezo,..najaribu kukuza vipaji ili tuungane na vyama vya mpira na viongozi wetu, tumleta Msemaji wa Simba  Ahmed Ally ili na yeye aone kuwa hata vijijini kina vipaji vya mpira kutoka kwa Vijana wetu" amesema.

Mwisho.





Post a Comment

0 Comments