WANAWAKE WAONYWA UFUGAJI WA FISI, WASISITIZWA KUOMBA KIBALI.

 Afisa Mwandamizi na Kamanda wa Pori la Akiba la Kijereshi, FloraVick Kalambo akitoa elimu ya uhifadhi kwa Wananchi wa Kijiji cha Mwantimba kata ya Matongo wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu.

‎Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

‎MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyapori Tanzania (TAWA) imewataka wananchi hususani akina mama kuacha mara moja tabia ya kufuga Wanyamapori hasa fisi kwa matumizi binafsi na badala yake wawakatie kibali kwani wakikamatwa wanafuga bila kibali watachukiliwa hatua kwa mujibu wa sheria.


‎Hayo yamebainishwa leo la Afisa Mwandamizi na Kamanda wa Pori la Akiba la Kijereshi, FloraVick Kalambo, wakati akitoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi wa vijiji Matongo, Masewa na Mwantimba ambavyo vinavyopakana na pori la Akiba Kijereshi na hifadhi ya Serengeti.



‎Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria, kumiliki Wanyamapori bila kibali ni Kosa la kisheria na ukikutwa na mnyama huyo, kifungo ni miaka 20 na pia wananchi hawaruhusiwi kufanya shughuli zozote za kibinadamu ikiwemo ufugaji, uwindaji wala kuokota kuni ndani ya hifadhi.

‎"Kuna changamoto kubwa ya wananchi wetu kumiliki rasimali Wanyamapori kinyume na Sheria, Rasirimali hizi zinamilikiwa zingine zikiwa hai na zingine ni viungo vya Wanyamapori... miongoni mwa wamiliki wa rasimali za Wanyamapori hai hususani fisi kwa lengo la kuwatumia kama chombo cha usafiri ni Wakina mama". Amesema.



‎Amesema kuwa kwa kutambua hilo, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania imetoa nafasi ya kuwafuga Wanyamapori hai ambao ni rafiki kwa binadamu huku akiwasihi akina mama kurejesha Mifugo hiyo porini sababu majumbani siyo sehemu yao na kwamba Kwa Mifugo inayoruhusiwa kufugwa watapewa kibali na miongozo juu ya ufugaji wake.

‎Amewataka pia baadhi ya wananchi wanaomiliki viungo vya Wanyamapori pori kwani kumiliki viungo hivyo ni sawa ma Ujangili ambapo aliwakaribisha kupewa kibali na kuhuisha vibali vyao kwa kazi mbalimbali ikiwemo utamaduni.



‎Amewataka wananchi kuacha kuingiza Mifugo hifadhini ili wasibebe magonjwa ya Wanyamapori pia watasababisha Simba waliozeeka kushambulia Mifugo yao.

‎Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga amewataka wananchi kuacha mara moja Ujangili huku akisisitiza kuwa serikali imejipanga kudhibiti Tembo kwa kujenga uzio wa fensi ya umeme maeneo ya mpakani.

‎Mwisho.




Post a Comment

0 Comments