POLISI YAWAONYA WAPIGA RAMLI CHONGANISHI.

Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Chacha Maro Mei 15,2026 amefanya mkutano na wananchi wa kijiji cha Ng'hesha Wilayani Itilima, kwa lengo la kukemea vitendo vya baadhi ya Waganga wa tiba asili kujihusisha na upigaji wa ramli chonganishi ambazo zinaweza kupelekea Mauaji, Majeruhi na hata kupelekea kusambaratisha familia.

Aidha, amewataka viongozi wa sungu sungu wasiwe sehemu ya uhalifu kwa kufanya vitendo vya kujichukulia sheria mkononi vitendo ambavyo ni uvunjifu wa sheria, amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia Mtu/Watu ambao watakiuka na kuvunja sheria na kanuni za Nchi.

Kwa upande wa Afisa Tarafa ya Kanadi Lameck Lupiga amewataka wananchi wa Kijiji cha Ng’hesha kufuata taratibu kwa kutoa taarifa mbalimbali sehemu husika na sio kujichukulia sheria mkononi.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Ng’hesha Bunga Nselema amelipogeza Jeshi la Polisi kwa kutoa elimu kwa wananchi wa kijiji hicho na amesema elimu hiyo itakuwa na manufaa makubwa sana kwao.

Mwisho.






Post a Comment

0 Comments