MAAFISHA USAFIRISHAJI MWIKA KUSINI, WATAKIWA KUWA WALINZI KATIKA JAMII.

 

Na Mwandishi Wetu Moshi.

MAAFISA usafirishaji (Bodaboda) katika kata ya Mwika Kusini wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wametakiwa kuwa walinzi wa amani na kupinga vitendo vya kihalifu vinavyoweza kuchafua taswira nzuri waliyojijengea.

Kauli hiyo imetolewa na diwani wa kata hiyo John Tarimo wakati wakuchangia ujenzi wa vibanda vya maegesho kwa watoa huduma hao katika vijiwe vya Mahakamani, Makerere na Marialle ambapo katika kila kijiwe kilipata mchango wa shilingi laki tatu.

Alisema kuwa huduma hiyo ni muhimu kwa jamii na inatakiwa kuendelea kufanyika kwa kufuata kanuni na taratibu bila kiwepo na uvunjifu wa amani katika jamii inayowahudumia.

Alisema kwa kipindi kirefu watoa huduma hao kwa sasa wamekuwa walinzi wa amani na kuwa hakuna malalamiko ambayo yametijokeza yakiwahusisha hivyo hawana budinkuendelea kuitunza heshima hiyo waliyojiwekea

Kwa mujibu wa Tarimo ni kuwa ugawaji wa fedha hizo ni utekelzaji wa ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni baada ya kupata kilio cha ukosefunwa vibanda vya kujikinga na jua ama mvua kwa bodaboda hao.

Hata hivyo aliwataka kuendelea kutafuta fursa nyingine za kiuchumi na kuwa ofisi yake milango ipo wazi katika kuwawezesha kuwasaidia na sio kuishia katika jambo moja pekee kwani miradi ya kiuchumi ipo mingi.

Deogratiis Mtui ni katibu wa waendesha bodaboda kijiwe cha mahakamani ambapo alimshukiru diwani huyo kwa kutekelezwa ahadi yake hiyo na kuwa fedha hizo zitaenda kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na sii vinginevyo.

Alisema kupatikana kwa vibanda hivyo kutaenda kuwaondolea adha waliyokiwa wakiipata hususan kipindi cha mvua au jua kwa kukosa sehemu sahihi ya kujisitiri wao pamoja na abiria.

Mwisho.






Post a Comment

0 Comments