WAZIRI WA KILIMO AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA PAMBA DODOMA.

 


Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.

WAZIRI wa Kilimo Daniel Chongolo amefungua Mkutano wa Wadau wa Pamba na kueleza kwamba serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan inashirikiana na Wadau wa sekta ya Kilimo katika utoaji wa huduma za ugani, pembejeo na Teknolojia.


Ameeleza kuwa Tasnia ya Pamba imeendelea kuimariasha huduma za Ugani kupitia Bodi ya Pamba Tanzania Kwa wakulima ambapo wanashirikiana na Kampuni za Pamba kuhudumia wakulima.


Amempongeza Rais Dk. Samia kwa juhudi zake za kuongeza na kuimarisha huduma za ugani zinazolenga kuongeza tija ya uzalishaji, kuongezeka kwa matumizi ya zana Bora za kilimo ambapo katika msimu huu jumla ya Trekta 780 zimesambazwa kwa Wakulima. 


Ameeleza kwamba wakulima wengi wa pamba nchini, ni wakulima wadogo wenye mashamba ya ekari moja au zaidi na bado wanakabiliwa na matumizi ya zana duni za kilimo na kuongeza kuwa Uwekezaji wa sekta ya Kilimo utaongeza tija ya uzalishaji. 


"Na ili kukabiliana na changamoto zilizopo, serikali inaendelea na Mipango yake ya kujenga bwawa la umwagiliaji katika shamba la Kanzinga kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu za pamba... Kuhusu upatikanaji wa mbegu, serikali umeweka utaratibu wa uchangiaji kupitia Mfuko wa CDTFambao unaongeza uzalishaji." Amesema Chongolo.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba, Christopher Gachuma, amesema kuwa Wakulima wa Pamba wanahitaji tija huku akitaja siri kubwa Iko kwenye tija huku akitolea mfano mwaka jana walilima ekari mil. 1, na kuzalisha kilo mil. 2.2.

"Hili jambo tumelizungumza kwenye Bodi, tuone namna wakulima wanavyoweza kupata Elimu, tumejiwekea wastani wa kilo 500 kwenye ekari moja yaa pamba ili kuajiri vijana wengi zaidi" amesema.


Mkuugenzi wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga amesema kuwa Pamba ni zao muhimu kwenye Uchumi na kwamba mnyororo wa Pamba umetumika kutengeneza ajira. 

Amefafanua kuwa serikali imefanya majaribio ya uimaerishaji utoaji wa huduma za ugani kupitia BBT ambapo mwaka 2023/24 walianaza na kata 40, mwaka 20224/25 walifikia kata 232 na mwaka 2025/26 walifikia kata 589.


Amesema kuwa hadi sasa hatua mbalimbali zimechukuliwa kuboresha upatikanaji wa mbegu Bora za Pamba ikiwemo kuimarisha utafiti wa mbegu za pamba ambapo vinasaba vya mbegu kutoka Pakistani vimeonyesha ufanisi katika kudhibiti jassids.

Mtunga ameeleza kuwa hadi sasa wameongeza uzalishaji wa mbegu mama na msingi (breeder na pre-basic) kwa kuweka miundombinu ya umwagiliaji ambapo jumla ya ekari 130 zimelimwa ukilinganisha na ekari 40 msimu uliopita, pia wanatarajia kusimika kiwanda cha kuchakata mbegu za pamba.


Mbunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga ameitaka serikali kupitia Wizara ya Kilimo kufanya kazi pamoja na wataalamu wa Kilimo ili uzalishaji wa Pamba uanzie ngazi ya chini huku akisisitiza kuwa hakuna mtu anayepingana na utaalamu.


Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka mikoa 17 inayolima pamba wakiwemo wakuu wa. Mikoa, Wakuu wa wilaya, wakurugenzi, Maafisa Kilimo, wazalishaji na wasambazaji wa mbegu, Wanunuzi wa Pamba, viongozi wa amcos, wakulima, watumishi wa Bodi ya Pamba na Waandishi wa Habari za Pamba.

Mwisho 



Post a Comment

0 Comments