Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.
MBUNGE wa Jimbo la Itilima Mkoani Simiyu, Njalu Silanga amewaongoza Wabunge wa Mkoa huo kushiriki Mkutano wa Wadau wa Pamba uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention (JKC) jijini Dodoma ambalo ulikuwa unajadili masuala ya Pamba.
Mkutano huo umefunguliwa leo na Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, ambapo pamoja na mambo mengine serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan inashirikiana na Wadau wa sekta ya Kilimo katika utoaji wa huduma za ugani, pembejeo na Teknolojia.
Chongolo ameeleza kuwa Tasnia ya Pamba imeendelea kuimarisha huduma za Ugani kupitia Bodi ya Pamba Tanzania Kwa wakulima ambapo wanashirikiana na Kampuni za Pamba kuhudumia wakulima.
Akichangia hoja katika Mkutano huo, Mbunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga ameitaka serikali kupitia Wizara ya Kilimo kufanya kazi pamoja na wataalamu wa Kilimo ili uzalishaji wa Pamba uanzie ngazi ya chini huku akisisitiza kuwa hakuna mtu anayepingana na utaalamu.
Njalu amewapongeza wakulima walioanza kuzalisha Pamba kwa tija huku wengine wakipewa zawadi na serikali ambazo zimeongeza motisha kwenye uzalishaji wa Pamba.
Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga amesema kuwa Pamba ni zao muhimu kwenye Uchumi na kwamba mnyororo wa Pamba umetumika kutengeneza ajira.
Amefafanua kuwa serikali imefanya majaribio ya uimaerishaji utoaji wa huduma za ugani kupitia BBT ambapo mwaka 2023/24 walianaza na kata 40, mwaka 20224/25 walifikia kata 232 na mwaka 2025/26 walifikia kata 589.
Wabunge wa Mkoa wa Simiyu waliohudhuria katika Mkutano huo ni Njalu Silanga (Itilima), Salum Khamis-Jambo (Meatu), Masanja Kadogosa (Bariadi vijijini), Musa Mbuga (Meatu), Mashimba Ndaki (Maswa Mashariki), Tinah Chenge na Ester Midimu (viti Maalumu) huku Mhandisi Kundo (Bariadi), Simon Songe (Busega) na Mhandisi Lugomela (Maswa Magharibi) hawakuweza kuhudhuria kutokana na majukumu ya Kibunge na kiserikali.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka mikoa 17 inayolima pamba wakiwemo wakuu wa. Mikoa, Wakuu wa wilaya, wakurugenzi, Maafisa Kilimo, wazalishaji na wasambazaji wa mbegu, Wanunuzi wa Pamba, viongozi wa amcos, wakulima, watumishi wa Bodi ya Pamba na Waandishi wa Habari za Pamba.
Mwisho.








0 Comments