VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA, TANZANIA YAPATA KONGORE: UNODC YAIPA TEKNOLOJIA YA KISASA

 

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imepokea vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa kimaabara kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), ikiwa ni pongezi  baada ya kutambua mafanikio yaliyofikiwa na  Tanzania  katika udhibiti wa dawa za kulevya nchini.
 
Pongezi hizo zimetolewa tarehe 22 Aprili 2026 jijini Dar es Salaam na ujumbe wa UNODC ukiongozwa na Mwakilishi wa  Kanda ya Afrika Mashariki, Ali El-Bereir, ambaye aliipongeza Tanzania kwa jitihada zinazofanyika katika kudhibiti biashara na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kemikali bashirifu.

Vifaa hivyo  hutokewa mahsusi kuzijengea uwezo taasisi zinazosimamia udhibiti wa dawa za kulevya katika ngazi ya kimataifa chini ya mpango wa Kimataifa wa Port Security and Safety of Navigation Programme (EU PSP). huo umetolewa chini ya mpango wa kimataifa wa Port Security and Safety of Navigation Programme (EU PSP).

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mashine za kisasa zenye uwezo wa kubaini kwa haraka aina mbalimbali za dawa za kulevya na kemikali zinazodhibitiwa hata zikiwa ndani ya vifungashio vyake bila kufunguliwa. Hivyo, kuwezesha ufanisi wa kichunguzi na kuboresha utendaji kazi wa Mamlaka. 

Aidha, UNODC imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo maafisa  wa DCEA ili kuimarisha mapambano.

Post a Comment

0 Comments