Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
ASKOFU wa Kanisa Katoliki , Jimbo jipya la Bariadi, Mhashamu Prosper Lyimo amewataka Wazazi na Walezi kuhakikisha wanasimamia malezi ya watoto ili waishi na kukua kwa kumjua Mungu.
Aidha Askofu Lyimo amesema Kanisa Katoliki linaendelea kulea jamii na watoto katika maadili ya kiroho (dini), kimwili (Elimu na afya) ili kuwa na Taifa lenye malezi mazuri.
Askofu Lyimo ameyasema hayo wakati wa homilia, aliyoitoa leo wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu iliyofanyika katika kigango cha Mt. Mathayo Kidinda huku akizitaka familia kudumisha wito wa ndoa ili kupata watumishi wengi shambani mwa bwana.
"Malezi ya watoto ni muhimu sana, majitoleo na kuleta familia katika wito wa ndoa ili kupata watumishi wengi shambani mwa bwana kupitia miito mitakatifu ya Upadre, Usista na watoto wakitaka kumtimikia Mungu muwaruhusu" amesema Askofu Lyimo.
"familia tuzingatia malezi na miito tusisitize katika familia zetu, mjiunge na vyama vya kitume, muwaruhusu watoto kujiunga na vyama vya kitume"
Askofu Lyimo ameeleza kuwa baada ya kusimikwa katika Jimbo hilo, mpaka sana Jimbo linayo Mipango mingi ya muda mfupi, wa kati na mrefu huku aliwa waumini na viongozi kushirikiana kuteleza Mipango hiyo.
Amwataka kuendeleza maeneo ya vigango na Parokia kwa kupanda miti, ili yasiporwe Wala kuchungiwa Mifugo huku akiwasisitiza kuweka Mpango wa kuongeza maeneo Kwa ajili ya huduma.
"tunatoa huduma kiroho na kimwili, tupange kuangalia kuongeza maeneo huko mbele miaka 20 ili tuendeleze kigango chetu, tunatembea kwa pamoja hatua Kwa hatua." amesema.
Kauli Mbiu ya Jimbo la Bariadi "Sala, Huduma, Haki na Amani"

0 Comments