POLISI mkoani Arusha, wanamshikilia mtu mmoja aitwaye Salmin Rajab (29) fundi ujenzi, mkazi wa Sinoni jijini Arusha, kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake aitwaye Sahiri Salmin mwenye umri wa miezi nane, aliyemchinja shingoni na kutenganisha kichwa na kiwiliwili.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo , Kamanda wa polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo, amesema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Aprili 28, mwaka huu majira ya jioni.
"Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha tunamshikilia Rajab kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake wa miezi minane...Tunaendelea na uchunguzi, upelelezi ukikamilika atafikishwa mbele ya sheria kwa hatua zaidi".
Jirani wa mtuhumiwa huyo, Mirium Kivuyo, ameema mtuhumiwa alitenda kosa hilo baada ya mke wake kwenda dukani kununua tambi za kupika akiwa na mtoto wao mwingine, aliporejea alikuta mlango umefungwa kwa ndani na alipogonga mume wake alifungua na kupiga magoti akiomba msamaha kwa madai kuwa ameua.
Source.
#uhuruonline

0 Comments