CCM YAMTEUA KAGANDA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA ISMANI.



CHAMA  Cha Mapinduzi (CCM), kimemtangaza Emmanuela Kaganda  kuwa mgombea katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Isimani, mkoani Iringa.

Uteuzi huo umefanywa leo Aprili 29, 2026 na Kamati Kuu ya CCM kwa mujibu wa mamlaka iliyoainishwa chini ya Ibara ya 105 (7)(f) ya Katiba ya chama ya mwaka 1977, toleo la Julai 2025.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Aprili 29, 2026 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani  Kihongosi, chama kimekamilisha mchakato wa kumpata mgombea wake atakayeiwakilisha CCM katika uchaguzi huo mdogo.

Source.

#uhuruonline

Post a Comment

0 Comments