RC SIMIYU ATETA NA WATUMISHI AJIRA MPYA BARIADI.

 


Na Mwandishi wetu, Bariadi,

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha, leo 29 Aprili 2026 amezungumza na Watumishi wa Ajira mpya wa Kada mbalimbali walioajiriwa katika Halmashauri mbili za Mji na wilaya ya Bariadi na kuwasisitiza juu ya Uzalendi, Uwajibikaji na kuzingatisa Maadili katika utumishi wa Umma.

Akizungumza  na Watumishi hao katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji iliyoko  Nyaumata Wilayani Bariadi, Macha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ajira nyingi kwa vijana Nchini.


"Huu ni Mwaka mmoja  tu Mhe.Rais Dkt.Samia Suhuhu Hassan ameleta ajira mpya Wilayani  Bariadi  pekee zaidi ya Watumishi 200 ni jambo kubwa linalopaswa kupongezwa"Alisema Mkuu wa Mkoa Mhe.Macha


Amesema kuimarika kwa uchumi kumeiwezesha Serikali kujairi watumishi wengi zaidi Nchini hatua itakayochochea kwa kiasi kikubwa utoaji wa huduma bora kwa Wananchi.


"Shukrani zenu zisiwe za mdomo wala nadharia na badala yake Shukrani zenu ziwe kwa vitendo na badala yake shukrani zionyeshe matokeo chanya katika maeneo wanayokwenda kufanya kazi" Alisisitiza mkuu wa Mkoa Mhe.Macha.


Amewataka watumishi hao kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria kanuni na Taratibu za utumishi wa Umma ili waweze kudumu katika utumishi wa Umma.


Amewahakikishia Watumishi hao kuwa Serikali Mkoani humo itakua nao karibu katika kuwaelekeza kwa karibu namna bora ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Aidha amewataka watumishi hao kuwa kiungo kati ya Serikali na Wananchi  katika maeneo yao ya kazi badala ya kujihusisha na uanaharakati unaopelekea kuichonganisha Serikali na Wananchi.

Mwisho.




Post a Comment

0 Comments