Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.
SERIKALI imesema kuwa itahakikisha inaifanyia marekebisho Barabara ya Bariadi kwenda Lamadi kupitia fedha za Mfuko wa Barabara.
Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tinah Chenge aliyeuliza, "Kwa kuwa barabara ya Kwenda Bariadi-Lamadi, imeharibika sana, ni upi Mpango wa serikali kuitengeneza Barabara hii muhimu Kwa Uchumi wa Mkoa wa Simiyu"?
Waziri Ulega alijibu, " Ni Ukweli, Barabara hii kubwa ya Bariadi-Lamadi ikiwa ni pamoja na Ile inayotoka Lamadi, Bunda mpaka Musoma... ni miongoni mwa Barabara zilizoharibika sana" .
"Nataka nimuhakikishie Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, mheshimiwa Tina Chenge kwamba, Barabara hii ni miongoni mwa Barabara tutakazozipa kipaumbele kwenye marekebisho kupitia Mfuko wetu wa Barabara" amesema na kuongeza.
"Na tunao Mpango Mkubwa waheshimiwa Wabunge mtauona wa kwenda kufanya marekebisho hayo makubwa wa kulipa nguvu Bodi ya Mfuko wa Barabara ili tufanye matengenezo kwa Barabara Kuu zote zile za kiuchumi, zibaZobeba Uchumi wetu ikiwemo hii ya Bariadi-Lamadi. "
Mwisho.





0 Comments