WATU sita wamepoteza maisha huku wengine 55 wakijeruhiwa kufuatia ajali ya basi la Kampuni ya Greenline iliyotokea katika Kijiji cha Mkiwa, Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Amon Kakwale, amesema ajali hiyo ilitokea wakati basi hilo lililokuwa likisafiri kutoka Dodoma kuelekea Mwanza lilipojaribu kukwepa shimo barabarani, hali iliyosababisha dereva kushindwa kulimudu na hatimaye kupinduka.
Amesema majeruhi wote 55 wamekimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya haraka, huku miili ya marehemu ikihifadhiwa hospitalini hapo ikisubiri taratibu nyingine.
Aidha, Kamanda Kakwale, huyo ameeleza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo kamili cha ajali, huku akitoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuwa makini wanapopita katika maeneo yenye changamoto za miundombino.
Source:
#uhuruonline



0 Comments