RAIS DKT. SAMIA ACHANGIA MIL. 50 JIMBO JIPYA LA BARIADI.

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan.

Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia  Suluhu Hassan ametoa kiasi cha shilingi Mil. 50 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa Katoliki Jimbo jipya la Bariadi Mkoani wa Simiyu. 

Akizungumza wakati wa kuwasilisha salamu za Rais Samia kwenye usimikwaji wa Askofu mpya wa Jimbo jipya la Bariadi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, AnaMringi Macha amesema Dhamira ya Rais ni kuziheshimu na kuzipenda Taasisi za dini hapa nchini wakati huohuo anasisitiza Upendo wa dhati kwa kanisa katoliki na viongozi na dini.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, AnaMringi Macha akiongea kwenye Misa ya kumsimika Askofu mpya wa Jimbo jipya la Bariadi.

Amesema Rais Samia ameendelea kutambua mchango wa taaisis za dini katika akujenga Taifa la Tanzania katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, huduma za kijamii, Mafundisho kiroho ambayo huzaa wananchi wema wanaoendelea kulinda amani yaa nchini

"Mhe,  Rais Bado anadhamira ya dhati kuendelea kushirikiana na kuzisaidia Taasisi za dini kwani anafahamu Ustawi wa taaasisi za dini ndio Ustawi wa Taifa letu...kwa kutambua kuwa sisi wa Bariadi tuko kwenye ujenzi wa kanisa kuua Bariadi, amenielekeza niwasilishe kwenu shilingi Mil.50 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa katoliki Jimbo la Bariadi" amesema.

Ameongeza kuwa, Rais Samia anaendelea kuzitaka Taasisi za dini kupitia madhehehu yake ziendeleee kuiombea Tanzania na viongozi wake ili ziendeleee kuwa na amani.

Macha amempongeza askofu Lyimo kwa kusimikwa kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo jipya ya Bariadi huku akiahidi kuwa serikali itaendelea kumpa ushirikiano wa kiwango cha juu kadri itakavyowezekana kwani wanaatambua ushirikiano unakuza amani.



Askofu wa Jimbo la Shinyanga, Mhashamu Liberatus Sangu, almevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuhakikisha jambo hilo la kitume linafanikiwa.

"Tunamshukuru Mungu, kwa yote anayotutendea, Falsafa ya Jimbo la Shinyanga ya kusogeza huduma imetimia, tunaishukuru Serikali na vyombo vya ulinzi na msaada mmekuwa muhimu katika utume wetu" amesema.

Akitoa homilia yake kwenye adhimisho la Misa Takatifu, Askofu wa Jimbo la Ruleng-Ngara, Mhashamu Severine Niwemugizi amesema kuwa kuanzishwa kwa Jimbo jipya la Bariadi ni alama ya kukua kwa kanisa na imani ambayo ni msingi wa matumaini.


Amesema kuwa Jimbo jipya la Bariadi limeanzishwa kwa wakati sahihi kwani idadi ya Parokia, wakrelo na waamini walei ni wengi ma hivyo huduma za kiroho zinatakiwa kuwa karibu.


Mwisho.







Post a Comment

0 Comments