FAMILIA YENYE MAPADRI WATATU, YATOA ASKOFU LYIMO.

 



Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

‎KATIBU Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Dk Charles Kitima amesema kuwa familia anayotoka Askofu Prosper Lyimo ilikuwa na Mapadri watatu, ambapo kati yao sasa  mmoja (Askofu Lyimo) ni Askofu wa Jimbo Jipya la Bariadi.


‎Padri Dk. Kitima pia amesoma rasmi hati ya kipapa kutoka kwa Baba Mtakatifu Leo XIV, kuthibitisha uteuzi wa Mhashamu Askofu Prosper Lyimo kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo jipya la Bariadi.

‎Baada ya usomaji wa hati hiyo, ibada ya kumsimika Askofu Lyimo ilifanyika rasmi, ambapo alikabidhiwa majukumu ya kuliongoza jimbo hilo jipya. Hafla hiyo iliongozwa na Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mwanza, Renatus Nkwande, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kanisa, waumini pamoja na wageni waalikwa.



‎Akitoa neno la Shukrani, Askofu Lyimo amesema Mashemasi na Mapadri wamewekwa kuwasaidia maaskofu ambapo amewataaka kushirikiana kufanya kazi kwa Upendo.

Amewataka watawa wote wa kike na wa kiume kuendelea kufanya kazi kwa pamoja huku akisisitiza kuwa waamini walei na vyama vya kitumie wana nafasi kubwa katika kanisa.

‎"nathamini utume wenu Mapadri watawa na walei, nitashirikiana nanyi Kwa moyo wa dhati tuombeane, tufanye kazi kushirikiana kila mmoja Kwa nafasi aliyonayo." amesema Askofu Lyimo.


‎mwisho.









Post a Comment

0 Comments