ENG. KUNDO AMKABIDHI ZAWADI YA MONSTRANCE ASKOFU LYIMO.

 

‎MBUNGE wa Jimbo la Bariadi Mjini, Mhandisi Kundo Mathew (kulia) akikabidhi zawadi ya Monstrance (chombo cha kuonyeshea ekaristi takatifu) kwa Askofu wa jimbo jipya la Bariadi, Mhashamu Prosper Lyimo.

Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


‎MBUNGE wa Jimbo la Bariadi Mjini, Mhandisi Kundo Mathew ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, amekabidhi zawadi ya Monstrance (chombo cha kuonyeshea ekaristi takatifu) kwa Askofu wa Jimbo la Bariadi Mkoani Simiyu, Mhashamu Prosper Lyimo.

‎Mhandisi Kundo amekabiddhi zawadi hiyo kwenye Adhimisho la Misa Takatifu ya kusimikwa kwa Askofu mpya wa Jimbo la Bariadi, Prosper Lyimo katika misa iliyofanyika Uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi.

‎Mhandisi Kundo amemshukru  Papa Leo XIV kwa kukubali Kuanzisha kwa jimbo jipya  katoliki Bariadi na kumsimika Askofu wa Kwanza wa jimbo katoliki la Bariadi, Mhashamu Prosper Baltazar Lyimo kwa lengo la kusogeza huduma za kiroho kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na kuleta mwanga wa Imani, tumaini na upendo kwa wote.



‎"Ni ngumu kuongea mbele ya Wana falsafa na wanateoelojia...Tunamshukuru mwenyezi Mungu mapenzi yake yametimia...tunashukuru baba Leo kutangaza Jimbo la Bariadi na kupata askofu mpya, Bariadi ina baraka, Rais Samia aligawa Jimbo ili kusogeza huduma kwa wananchi" amesema na kuongeza.

‎"kugawanya Jimbo ni kusogeza huduma za kiroho karibu na wannachi, tunamashukuru Mungu Kwa zawadi ya huduma ya kiroho, Usingizi wako ulete mwanga wa imani"

‎Monstrance ni chombo cha kuonyeshea ekaristi takatifu, jina hilo limetokana na lugha ya kilatini.

Mwisho.














Post a Comment

0 Comments