Mbunge wa Jimbo la Bariadi mjini, Mhandisi Kundo Mathew ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, akisalimia na Shekhe wa Mkoa wa Simiyu, Issa Kwezi.Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
WAUMINI wa dini ya kiisalamu wametakiwa kuwalinda na kuwalea watoto na vijana katika misingi ya dini na Elimu dunia ili kujenga jamii imara na yenye misingi thabiti.
Aidha kupitia mafundisho ya dini watajenga jamii yenye unyenyekevu na kuwekeza katika matendo mema ili kujenga Taifa zuri lenye misingi ya imara.
Hayo yamebainishwa leo na Mbunge wa Jimbo la Bariadi mjini, Mhandisi Kundo Mathew ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, wakati akitoa msaada wa vyakula katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, katika Msikiti wa Ijumaa na kusema kuwa Taasisi za dini na serikali zinawekeza katika sekta ya Elimu.
"Serikali ya Rais Dkt. Samia imewekeza katika sekta ya Elimu, vitendea kazi na walimu, tusisite watoto kupeleka Shule" amesema
Mhandisi Kundo amewataka waumini na viongozi wa dini kuendelea kuombea amani na utulivu, pia kuwaombea viongozi wa kitaifa ili waendelee kufanya kazi kwa mapenzi ya Mungu.
Amesema kuwa amani ya nchi inatokana na swala na sala na kwamba bila utaratibu wa kuswali watenda zambi na uhalifu hautapungua.
Shekhe Mkuu wa Mkoa, Isa Kwezi amesema katika dini ya uislamu Elimu ni lazima na siyo hiari kwa Wanawake na wanaume.
Amesema kuwa pamoja na Elimu za madrasa zinazofundisha madili, heshima, busara na adabu katika Elimu ya dini. na kusisitiza kujifunza Elimu ya Mazingira.
"Baraza kuu la Waislamu (Bakwata) ni moja ya Taasisi inayosomesha Elimu ya Mazingira ili kujenga jamii yenye watu waadilifu." amesema.
Katika msaada huo, Mhandisi Kundo ametoa mchele kilo 300, sukari kilo 400, na tende kilo 100.
MWISHO.













0 Comments