Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji (kushoto) akisalimia na Askofu Mteule wa Jimbo la Bariadi Mhashamu Prosper Lyimo (kulia), katikati ni Askofu wa Jimbo la Shinyanga, Mhashamu Liberatus Sangu.
Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
ASKOFU Mteule wa Jimbo Katoliki la Bariadi, Mhashamu Prosper Lyimo amepokelewa Kwa shangwe na vigerege mara baada ya kuwasili mkoani Simiyu akitokea Mkoani Shinyanga.
Askofu Lyimo amepokelewa na viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji.
Baada ya mapokezi hayo katika Kijiji cha Zanzui wilayani Maswa Mkoani Simiyu, msafara huo ukaelekea kanisa la Mt. Luka na baadae wataekelea kanisa la Mt. John (Somanda) kwa ajili ya masifu ya jioni.
ASKOFU Mteule wa Jimbo Katoliki la Bariadi, Mhashamu Prosper Lyimo, akibusu ardhi ya Jimbo la Bariadi Mkoani Simiyu, kama ishara ya kuingia jimboni.
ASKOFU Mteule wa Jimbo Katoliki la Bariadi, Mhashamu Prosper Lyimo (kushoto) akisalimiana na Padri Paul Fagan, Paroko wa Parokia ya Nkololo.













0 Comments