Mzee Mhuli Ngeleja Enzi za uhai wake.
Na Mwandishi wetu Maalumu.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Mhuli Ngeleja amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa huo, Lumeni Mathias imeeleza kuwa msiba huo umetokea Machi 18, 2026 na kwamba Mwenyekiti huyo atakumbukwa kwa mchango wake katika ujenzi wa Chama na shughuli zingine za Maendeleo.
SAKAGOI BLOG, Tunatoa pole za dhati kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wanachama wote wa CCM Wilaya ya Itilima katika kipindi hiki kigumu, tunawaombea moyo wa subira na ustahimilivu.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
Mwisho.

0 Comments