MV, MWANZA YAPATA AJALI RC ATOA AFAFANUZI.

Na CHAUSIKU SAID,

Sakagoiblog, MWANZA.

MKUU wa Mkoa wa Mwanza Salum Hamduni ametoa ufafanuzi wa awali kuhusiana na tukio la Meli ya Mv. Mwanza kukwaruza mwamba Ziwa Victoria wakati wa majaribio majira ya saa nne asubuhi

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 18, 2026 baada ya tukio hilo katika Bandari ya Mwanza Kusini ambapo Meli hiyo imepaki.

Hamduni ameeleza Kuwaiti Meli hiyo ilikuwa kwenye utaratibu wakawaida wa majaribio kwaajili ya matayarisho ya kuanza safari zake.

"Meli ya Mv.Mwanza ilikuwa imepaki hapa Bandari ya Mwanzakusini laikini kwaupande wa Serikali kipitia Shirika la Meli Tanzania (TASHICO) walikuwa wako kwenye maandalizi ya awali ya kuona namna ya kuanzisha safari za meli hiyo kwa bahati mbaya ndipo tukio Hilo likatokea na mpaka sasa wataalamu wamefanya uchunguzi na meli yetu Iko salama"

Aidha, amesema kuwa wameshafanya mawasiliano na Wizara ya Uchukuzi na maelekezo ya Serikali ni kufanya uchunguzi wakina kwa lengo la kujua sababu halisi pamoja na madhara ambayo yameweza kujitokeza.

"Meli hii imepaki hapa na iko salama lakini tubataka kujihakikishia usalama zadi kwakufanya uchunguzi wa kitaalamu,timu ya wataalamu itaundwa kwakushirikiana na Wizara pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama,mamlaka za Serikali pamoja na wataalam ili uchunguzi huo ufanyike"

Ameeleza kuwa mara baada ya uchunguzi kukamilika Serikali kupitia Wizara husika na Mkoa watarudi kutoa taarifa ya kina kwa wananchi, huku akiongeza kuwa timu hiyo itafanya kazi ndani ya siku kumi na nne na majibu yatakuwa yamepatikana.

Ndani ya Meli hiyo kulikuwa na wataalamu wa Wizara ya Uchukuzi ambao kwa namna moja au nyingine wanahusika moja kwa moja na suala zima la uendeshaji na ushauri wa Shirika la TASHICO.

Mwisho. 






Post a Comment

0 Comments