Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.
SERIKALI kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema kuwa Thamani ya ardhi hutumika kukadiria ada na tozo mbalimbali zinazohusika katika ukamilishaji wa miamala ya ardhi ikiwemo Kodi ya pango ya ardhi.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kaspar Mmuya wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge ambaye aliuliza Je, Kwa Nini wananchi wanatozwa riba ya pango la ardhi kuanzia mwezi Januari hadi juni badala ya kuanza kutozwa unapoanza mwaka wa serikali?.
Naibu Waziri huyo amesema, Sera ya Taifa ya ardhi ya mwaka 1995, Toleo la 2023 inatambua kuwa ardhi Ina thamani na thamani hiyo inapaswa kutambuliwa na kukaguliwa Kwa kuzingatia aina ya matumizi mahali eneo ilipo, kiwango cha Uendelezaji wa eneo na uwepo wa Miundombinu mbalimbali katika maeneo husika.
Alieleza kuwa kodi ya pango ya ardhi huanza kutozwa Kwa kipindi Cha mwaka wa fedha kuanzia tarehe 1 Julai kila mwaka katika kipindi chote Cha umiliiki.
"Kwa mujibu wa sheria, mmliki ana wajibu wa kulipa Kodi ya pango Kwa hiari ndani ya kipindi Cha miezi sita ya mwaka wa fedha ili kuwezesha Utekelezaji wa mipango ya serikali kwa mwaka wa fedha husika, hivyo kifungu cha 35 cha kifungu kidogo cha 11 Cha Sheria ya ardhi sura ya 113 limeweka utaratibu kuwa endapo Kodi haitalipwa, ndani ya miezi sita baada ya tarehe ambayo ilipaswa kulipwa riba ya asilimia 0.5 Kwa mwezi italipwa kwenye kiasi ambacho hakijalipwa". Amesema.
Mwisho.






0 Comments