POLISI WAPELELEZI (CID) WATEMBELEA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU BUSEGA.

Na Mwandishi wetu.

MKUU wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Chacha Maro Septemba 05, 2026 amewaongoza Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Vyeo mbalimbali wa ofisi ya Upelelezi Mkoa wa Simiyu kutembelea katika Shule ya Msingi Bethany iliyopo Wilaya ya Busega ambayo ni shule yenye Wanafunzi mahitaji maalum.

Aidha, ACP Maro ametoa pongezi kwa MkurugeI wa kituo hicho cha kulelea watoto hao kwa kuwalea vyema kwani inapelekea watoto hao kukua katika malezi yalio bora na kuwafanya wajiepushe na vitendo vya uhalifu.

Pia amesema Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na jamii katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kuinganisha jamii na jeshi la Polisi, na wametaka wasisite kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu hasa vitendo vya ukatili kwa watoto hao waliopo katika shule hiyo.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa kituo hicho cha The Bethany Project Jesca James Paul amesema ametoa shukurani za kipekee kwa ujio wa wageni hao na amesema wanaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi ikiwa ni samba samba kwa kutoa taarifa za uhali na wahalifu.

Aidha, akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake Theresia Masalu ametoa shukurani kwa msaada huo uliotolewa na Jeshi la Polisi kwani umekuwa ni sehemu ya kurudi tabasamu kwao.

Mwisho.















Post a Comment

0 Comments