Masunga Keya Masunga (kulia) akiwa amemshika mkono Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Saidi Mtanda, kushoto ni Buhimila Shala pamoja na Waganga wengine wakishiriki kumsimika Mkuu huyo wa Mkoa na kumpa jina la Ndaturu Masanja.
Na Costantine Mathias, Bariadi.
MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Said Mtanda amekutana na Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala Mkoa huo leo Sept 5, 2016 na kusimikwa jina la Ndaturu Masanja.
Kwa mujibu wa Mila ya kabila la Kisukuma, Ndaturu Masanja maana yake ni Mtemi au Chifu anayeongoza na kuunganisha au kukusanya watu.
Akizungumza wakati wa kumtawaza Utemi Mkuu huyo wa Mkoa, Mwenyekiti wa Utamaduni Mkoa wa Simiyu Buhimila Shala amesema kuwa Mtemi Ndaturu Masanja alikuwa ni mtemi alitawala eneo la ntuzu na alipotawala watu walimsikiliza.







0 Comments