MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha (wa tatu kushoto) akikata utepe kwenye mitambo kwa ajili ya uzinduzi wa Ukarabati wa Bwawa la Nyangokolwa.Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
SERIKALI imetoa kiasi cha shilingi Bil. 1.012 kwa ajili ya Ukarabati wa Bwawa la Nyangokolwa ambalo linatarajia kunufaika wakazi 3,000 na Mifugo zaidi ya 5,000 huku Maji yake pia yakitumika kwa shughuli za kilimo cha Umwagiliaji.
Hayo yamebainishwa leo (August 4, 2026) na Mkurugenzi wa Bonde la Ziwa Victoria, Dk. Renatus Shinhu wakati akiwasilisha taarifa ya Ukarabati wa Bwawa hilo ambapo amesema kazi ya Mamlaka ya Bonde katika kuteleza majukumu yake ni pamoja na Usimamizi, Uendelezaji wa Rasilimaji za Maji na kuboresha maisha ya Wananchi.
Amesema kuwa bwawa la Nyangokolwa litakarabatiwa na litakuwa na uwezo wa kuhifadhi ujazo wa Lita za maji Milioni 212 ambapo litatatua changamoto ya upatikanaji wa Maji kwa wananchi pamoja na mifugo.
"Bwawa hili litaimarisha upatikanaji wa maji na kuongeza ustahimilivu wa ukame...Mradi huu utatekelezwa Kwa Force akaunti kwa gharama shilingi Bil. 1.012 na utatekelezwa kwa siku 60 sawa na miezi miwili kuanzia Sasa" amesema Dk. Shinhu.
Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew amesema Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ilimwelekeza Waziri wa Maji (Jumaa Aweso) kutoa fedha hizo kwa ajili ya Ukarabati wa bwawa la Nyangokolwa.
Amesema kuwa Bwawa hilo lina manufaa makubwa kwa wananchi ikiwemo matumizi kunywa pamoja na kujenga mabarika (mbauti) ya kunyeshwea mifugo ambapo zaidi ya Mifugo 5,000 itanufaika pia litatumika kwa shughuli za kilimo cha Umwagiliaji ili wananchi waweze kujikwamua kiuchumi.
"Mradi huu unatekelezwa na Wataalamu wa Wizara ya Maji ambao wamewezeshwa, mitambo imetolewa na Rais Dk. Samia kupitia Kodi za Watanzania ambapo amenunua mitambo seti kwa ajili ya kujenga Mabwawa, pia kuna mitambo 25 imenunuliwa na kila Mkoa ina mtambo kwa ajili ya kuchimba Maji chini ya ardhi.. tunamshukuru sana Rais Dk. Samia kwa maamuzi ya kutazama sekta ya Maji na kununua mitambo kuwezesha sekta hii." amesema.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa miradi ya Maji, Wananchi watakuwa na uhakika wa huduma ya Maji na kwamba Rais ameshajipanga kuendelea kuinua vyanzo vya Maji na kuweka Mikakati ya kulinda vyanzo vya Maji ili view endelevu huku akiwahakikishia kuwa wako tayari kushirikiana na Wananchi kulinda chanzo hicho cha Maji.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ambaye ni, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, AnaMringi Macha amesema miradi mingi imekuwa haiendelei kutokana na sababu ya udokozi ambapo ameonya kwamba serikali itahakikisha miradi hiyo inasimamiwa kikamilifu bila kuhujumiwa.
"Miradi mingi inashindwa kuendelea kwa sababu ya udokozi, tutahakikisha tunachunga miradi kwa sababu tumebaini wizi unafanywa na Watu walioajiriwa ndani ya Mradi...tulinde hizi Mali ili miradi hii iweze kutunufaisha sote." amesema Macha.
Kwa upande wao wakazi wa Nyangokolwa, waliipongeza serikali kwa kukarabati bwawa la Nyangokolwa ambalo lilikuwa chanzo cha Maji kwa binadamu na Mifugo pia liliwasaidia wananchi kujiongezea kipato kupitia Kilimo cha Umwagiliaji.
Eleni Gabuga, mkazi wa Nyangokolwa alisema Ukarabati kwa Bwawa hilo, wananchi watajinufaisha na shughuli za kilimo na kuongeza vipato kupitia Kilimo cha Umwagiliaji.
Naye Marco Zacharia amesema kupitia Bwawa hilo wananchi watanufaika na kilimo cha Umwagiliaji, watajiongezea vipato pia wataweza kupata Maji kwa matumizi ya nyumbani.
Mwisho.















0 Comments