Diwani wa Kata ya Sima, Zebedayo Kingi (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wakipokea mifuko ya saruji iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mjini Mhandisi Kundo Mathew, kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Nkenyenge Charles.Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MBUNGE wa Jimbo la Bariadi Mjini, Mhandisi Kundo Mathew amekabidhi Saruji 247 pamoja na Mabati 60 ili kuwaondolea wananchi adha ya Kuchangia Maendeleo katika sekta ya Elimu.
Mhandisi Kundo amehitimisha ziara yake ya Kata kwa Kata kwenye Jimbo lake lenyr kata kumi, ziara ambayo ililenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoa Simiyu.
Mbunge huyo amekabidhi mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya ujenzi wa matundu 16 ya vyoo Shule ya Sekondari Biashara pamoja na Mabati 60, hatua ambayo inalenga kuboresha Mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi.
Pia amekabidhi mifuko 147 Kwa ajili ya kukarabati Vyumba vya madarasa sima Shule ya msingi ili kuboresha Mazingira ya ufundishaji, na kuhakikisha wanafunzi wanapata Elimu katika Mazingira mazuri.
Awali wananchi wamesema Idara ya ardhi imekuwa chanzo cha migogoro ya ardhi pamoja na utoaji wa hati za viwanja jambo ambalo linakwamisha ukuaji wa mji na Wananchi kufanya Maendeleo.
Musa Henry, Mkazi wa Lyalu kata ya Sima amesema baadhi ya Maafisa ardhi wanashirikiana na Madalali kuuza viwanja na maeneo ya watu jambo ambalo linasababisha migogoro ya ardhi ambayo haina ulazima.
Kaimi Afisa Ardhi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Magreth Ng'waka amesema zoezi la upimaji wa viwanja lishirikisha wananchi pamoja na viongozi wa Mitaa, huku akiahidi kufuatilia malalamiko ya wananchi hao.





0 Comments