TINA CHENGE AZUNGUMZIA CHANGAMOTO YA MUINDOMBINU YA WALEMAVU SIMIYU GIRLS.

 

‎MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge akiuliza swali Bungeni leo Juni 4, 2026.

‎NA COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.

‎MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge ameiomba serikali kutatua changamoto ya miundombinu wezeshi hasa nyakati za Mvua kwa wanafunzi wenye Ulemavu wanaosoma katika Shule ya Wasichana ya Simiyu (Simiyu Girls) iliyopo Igegu wilaya ya Bariadi.

‎Akiuliza swali Bungeni leo, Juni 4, 2026, Mbunge huyo alisema, "Kwa kuwa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Simiyu, Ina wanafunzi ambao wana ulemavu, Je ni lini serikali itatatua changamoto ya miundombinu wezeshi ili wanafunzi Hawa waweze kwenda madarasani hasa kipindi cha mvua ?."

Naibu Waziri TAMISEMI, Dk. Jaffar Seif akijibu swali Bungeni.

‎Akijibu Swali la Mbunge huyo, Naibu Waziri TAMISEMI, Dk. Jaffar Seif amesema miundombinu katika shule na kwenye  jamii imejengwa ili kuwezesha Kusaidia walemavu kupata huduma bila kikwazo chochote huku akimwelekeza Mkurugenzi wa Elimu kutembelea shule hiyo ili kubaini changamoto hiyo na awze kuchukua hatua.

‎"Mheshimiwa Spika, miundombinu ya shule na miundombinu inayotoa huduma katika jamii zetu, zote ni zimejengwa ili ziweze Kusaidia walemavu katika jamii zetu" amesema na kuongeza.

‎"Mheshimiwa Spika, nimwelekeze Mkurugenzi afike katika Shule ambayo Mheshimiwa Mbunge ameianisha ili kujiridhisha kama Miundombinu hii haipo na kama haipo achukue hatua za dharura kuweka miundombinu ili vijana wetu walemavu ambao wanapata Elimu katika Shule hii, wapate Elimu bila shida yoyote.".

‎Mwisho.




Post a Comment

0 Comments