Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge akiuliza swali Bungeni.
Na COSNTINE MATHIAS, Dodoma.
NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mary Prisca Mahundi, amesema kuwa kazi kubwa ya Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Halmashauri ni kumsha Ari, Kuchechemua pamoja na kuwatia moyo Wafanyabiashara wadogo ili waweze kuelekeza fedha za mikopo kwenye Malengo yaliyokusudiwa.
Naibu Waziri Mahundi ameyasema hayo leo Juni 18, 2026, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge aliyetaka kujua juu ya Mikakati ya serikali kufuatilia mikopo ili iweze kutumika kwa lengo lililokusudiwa.
NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mary Prisca Mahundi akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge.
Tina Chenga aliuliza, "Kwa kuwa hivi karibuni Tumeshuhudia Wanawake wa Mkoa wa Simiyu wakipatiwa mikopo, Kwa Mfano kwenye Halmashauri ya Bariadi vijijini na Mjini, serikali Ina Mkakati gani wa kufuatilia kama mikopo hii inatumika Kwa lengo lililokusudiwa ili iweze kurudishwa Kwa wakati?.."
Naibi Waziri akajibu, "Nikupongeze dada yangu Tina Chenge kwa swali zuri na ufuatiliaji wa karibu sana katika masuala haya, Mheshimiwa Naibu Spika kwenye jibu langu la msingi nilieleza kwamba Mikopo hii kabla ya kutolewa, utaratibu unaanza Kwa kutembelewa na Kutathimini aina ya Biashara ambayo huyu mwombaji anaenda kuifanya.
"vile vile wanapewa mafunzo ya Usimamizi wa fedha, lakini pia wanapewa namna njema ya kuelekeza kwenye malengo, kule kwenye maeneo yao Maafisa wa benki wanawafuatilia kuhakikisha wanaelekez fedha kwenye malengo, pia tunao Maafisa Maendeleo ya jamii kwenye maeneo haya kazi yao kubwa ni kuchechemua lakini pia kuamsha Ari na kuhakikisha kwamba wanaendelea kuwatia moyo Wafanyabiashara wadogowadogo kuelekeza fedha kwenye malengo" amesema na kuongeza.
"Kwa hiyo hii tutaendelea kuifanyia kazi na kuwasisitiza Maafisa ambao tunashirikiana nao kutoka kwenye mabenki lakini hasa Maafisa Maendeleo wetu hili ni jukumu lao mama."
Mwisho.





0 Comments