TINA CHENGE AHOJI KODI ZA MAJENGO KUTOZWA KWA NJIA YA LUKU.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge aakiuliza swali Bungeni.

Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.

SERIKALI kupitia Wizara ya Fedha imesema kuwa kwa Sasa Serikali inatumia viwango Mfuto kutoza Kodi za majengo kupitia Mita za Umeme za Luku.

‎Hayo yamebainishwa leo Juni 5, 2026 na Naibu Waziri wa Fedha, Laurent Luswetula wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge kupitia swali la msingi alilouliza, Je, Serikali inatumia kigezo gani katika kutoza Kodi ya majengo (Property Tax) kupitia mfumo wa Mita za Luku nchini?.

Naibu Waziri wa Fedha, Laurent Luswetula wakati akijibu Bungeni.

‎Akijibu Swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Naibu Waziri huyo alitaja vigezo vinavyotumika kutoza majengo kupitia Luku ni kama ifuatavyo, Nyumba ya kawaida ambayo inatozwa shilingi 18,000/= kwa mwaka au Shilingi 1,500/= kwa mwezi na nyumba ya ghorofa ambayo inatozwa shilingi 90,000/= kwa kila sakafu kwa mwaka au Shilingi 7,500/= kwa kila sakafu kwa mwezi.  Mheshimiwa Mwenyekiti, nyumba ya nyasi, udongo huduma za jamii (kuabudia) na wanayoishi Wazee kuanzia miaka 60 hazitozwi Kodi ya majengo isipokuwa endapo majengo hayo ni ya kibiashara.


‎Katika Maswali madogo ya nyongeza, Tina Chenge aliuliza, Kwa kuwa Kodi hii ya property Tax, inapaswa kulipwa na Mmiliki wa Jengo na kwa kuwa kuna wajasiriamali wamepanga kwenye fremu za Maduka yanayomilikiwa na wafanyabiashara na kwenye fremu hizi zimefungwa Luku, Kwa nini serikali inawakata property Tax wajasiriamali hawa kwenye Mita hizi za Luku? na Je, Serikali haioni haja na umuhimu wa kupitia upya ili Mmiliki wa Jengo huyu alipe Kodi hii kupitia Mita ya Luku badala ya kumbebesha mzigo mjasiriamali huyu,

Naibu Waziri alijibu, "Nimshukuru Tina Endrew Chenge, na kuendelea kuwapongeza Wanawake wa Mkoa wa Simiyu kwa kutuletea mtu makini na Bora ambaye anajenga hoja za kujenga hapa Bungeni.

‎"Kama serikali niweze kukiri kabisa Kwa Sasa hivi utaratibu unaotumika ndio huo Mheshimiwa Tina ameuzungumza kwamba inalipwa kupitia Luku, ambapo watumishi wa Luku ndio wanalipa na watumiaji wa Luku hawa wanaweza kuwa wamiliki au wanaweza kuwa wapangaji" amesema na kuongeza.

‎"Kwa upande wa wapangaji tumeliona hili kama serikali  na sisi Kwa kushirikiana na wenzetu ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI ambao ambapo hizi Halmashauri ziko chini yao, tumekaa na tumechakata na kuona namna Bora zaidi ambayo tutakusanya Kodi kwa wamiliki na siyo wapangaji."

Mwisho.





Post a Comment

0 Comments