TANESCO WAPELEKA UMEME BUNAMHALA SEKONDARI.

Nguzo za Umeme zikiwa zimesimikwa Shule ya Sekondari Bunamhala.

Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

SHIRIKA la Umeme (TANESCO), Mkoa wa Simiyu limepeleka na kufikisha Umeme Shule ya Sekondari Bunamhala iliyoko mtaa wa Songambele Halmashauri ya Mji wa Bariadi, kufuatia Ombi la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa huo, Tina Chenge aliyemwomba Waziri wa Nishati kufikisha huduma hiyo shuleni hapo.

Katika ombi lake, Mheshimiwa Tina Chenge, aliiomba serikali kufikisha huduma hiyo ya Umeme ili wanafunzi waweze kusoma katika Mazingira mazuri, Naibu Waziri wa Nishati akitoa siku tano (jumatatu mpaka ijumaa) kufikisha Umeme shuleni hapo, Tanesco Mkoa wa Simiyu wamefikisha na kuwa Umeme shuleni hapo.

Tazama picha hapa chini.













SAKAGOIBOG TULICHAPISHA HABARI HII WIKI MOJA JUMATATU NA UTEKELEZAJI UMEFANYIKA KWA MUDA MWAFAKA, HONGERA MWA MAMLAKA NA MUIBUA HOJA (MHE. TINA CHENGE).


HABARI ILIKUWA HIVI ..


SERIKALI YAMPA SIKU TANO TINA CHENGE KUPELEKA UMEME BUNHAMALA SEKONDARI.

Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba swali Bungeni.

Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.

‎WIZARA ya Nishati imemhakikishia Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge kuwa itafikisha umeme katika Shule ya Sekondari Bunamhala iliyoko mtaa wa Songambele Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani humo ndani ya siku tano kuanzia leo Juni 8, 2026.

‎Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba wakati akijibu swali na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge aliyetaka kujua, Ni lini Shule hiyo itapatiwa Umeme ili wanafunzi waweze kusoma katika Mazingira mazuri.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge akiuliza swali Bungeni leo Juni 8, 2026.

‎Mbunge huyo ameuliza "Kwa kuwa ni sera. ya serikali kupeleka Umeme kwenye Taasisi za umma, na Kwa kuwa Shule ya Sekondari ya Bunamhala iliyoko mtaa wa Songambele Bariadi, hakuna Umeme, Je ni lini serikali itapeleka Umeme kwenye Shule hii ili wanafunzi waweze kusoma?..." 

‎Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nishati, Makamba amesema, "Kwanza nimpongeze mama yangu, mama Tina Chenge umekuwa na bidii sana umekuwa ukitushauri kuhakikisha Mkoa wa Simiyu unapata Umeme wa uhakika lakini pia tunafikia Taasisi nyingi za Serikali," 


"Mheshimiwa Mbunge nikuhakikishie mpaka kufika ijumaa ya wiki hii, hiyo Shule itakuwa umepata umeme, Namwelekeza Meneja wa Tanesco Mkoa wa Simiyu kuhakikisha Taasisi zote za serikali zinapata Umeme ili tije ya Uwekezaji ionekane katika Taasisi hizo maana serikali ni moja na tunazungumzia pamoja, by Friday shule itakuwa imepata umeme." amesema.

‎Mwisho.






Post a Comment

0 Comments