MWENYEKITI SENETI YA VYUO VIKUU SIMIYU, AHIMIZA WANAFUNZI KUONGEZA JUHUDI ZA MASOMO. ‎

 

Na COSTANTINE MATHIAS.

MWENYEKITI wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Simiyu, David Wambura amewataka wanafunzi kujenga nidhamu na kuongeza jitihada shuleni na nyumbani ili waweze kufikia malengo yao kielimu.

‎Wambura ameyasema hayo juzi alipokuwa Mgeni Rasmi kwenye sherehe za kukaribisha wanachama wapya wa Skauti Biashara Sekondari, ambapo amewataka wanafunzi hao kuonyesha nidhamu na ushirikiano baina yao na walimu, wazazi na walezi.


‎"Ushiriki wetu katika hafla hii muhimu unaendelea kuonesha dhamira ya Skauti kuhamasisha vijana katika misingi ya Uzalendo, Uwajibikaji, Nidhamu na uongozi bora kwa maendeleo ya Taifa letu...vijana tujitume, tusome kwa bidii ili kufikia malengo yetu" amesema.

‎Amewata vijana hao kuendelea kuwa mfano wa maadili mema katika jamii, pia kuendelea kuwa walinzi wa rasimali na tunu za Taifa.

‎Awali kwenye risala waliyosoma mbele ya mgeni rasmi, wana chama wa Skauti Biashara sekondari waliomba kushiriki katika mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ngazi ya Halmashauri na shughuli zingine za scauti ndani ya Shule ikiwemo ulinzi na usalama wa Mali za shule.



‎Pia walitaja baadhi ya changamoto ikiwemo uelewa hafifu wa wazazi kuhusu chama Cha scauti, ulipaji duni wa ada za Skauti Taifa na mahudhurio duni ya wanachama ambapo wakimwomba Mwenyekiti huyo kuwachangia fedha za kuendeshea Mradi wa kutengeneza sabuni.

‎mwisho.





Post a Comment

0 Comments