TINA CHENGE AZUNGUMZIA UJENZI KIWANJA CHA NDEGE IGEGU.



Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.

SERIKALI kupitia Wizara ya Uchukuzi imesema kuwa inaendelea kufanya upembuzi yakinifu (Phisibility study) ili kujenga kiwanja cha ndege Igegu kilichopo wilayani ya Bariadi Mkoani Simiyu.

‎Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge aliyetaka kufahamu ni lini serikali itaanza kujenga uwanja huo muhimu kwa Uchumi na utalii wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge.

‎Tina Chenge aliuliza "kwa kuwa ni muda mrefu wananchi wa Kijiji cha igegu-Bariadi, wameachia maeneo yao kupisha ujenzi wa kiwanja cha ndege Cha Mkoa wa Simiyu, na Kwa kuwa hawaruhusiwi kuyaendeleza maeneo hayo, Je ni lini serikali itaananza kujenga uwanja huo muhimu Kwa Uchumi na utalii wa mikoa ya Kanda ya Ziwa?.. "
         Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina                             Chenge aakiuliza swali Bungeni.

Katika majibu yake Waziri Mbarawa amesema "Ni kweli wananchi wa Mkoa wa Simiyu wametoa baadhi ya maeneo Kwa ajili ya kujenga kiwanja cha ndege, Kwa Sasa Serikali unafanya upembuzi yakinifu ili kuona jinsi Gani tunaweza kujenga kiwanja hicho na kiwe na ukubwa gani na baada ya hapo tutatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja hicho."

‎Mwisho.


Post a Comment

0 Comments