Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
SERIKALI imeahidi kupeleka mtaalamu wa mifupa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu (Nyaumata) ili wananchi waweze kupata huduma hiyo ya kibingwa karibu na maeneo yao.
Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Dr. Florence Samizi wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge aliyetaka kufahamu kuwa lini serikali itapeleka Daktari Bingwa wa Mifupa?
" Kwa kuwa Hospitali ya Mkoa wa Simiyu, ni Hospitali ya Rufaa, na Kwa kuwa Hospitali hii haina Daktari Bingwa wa Mifupa, Je ni lini serikali itapeleka Daktari Bingwa wa Mifupa" aliuliza Mbunge huyo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge akiuliza swali Bungeni.
Akijibu swali hilo, Dr. Samizi alimpongeza Mbunge Tina Chenge kwa kuwapigania wananchi wa Mkoa wa Simiyu na kueleza kuwa "Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu ni moja ya Hospitali zinazotoa huduma za kibingwa na hospitali hii inatoa huduma za kibingwa sita" alisema na kuongeza.
"Naomba nimthibitishie Mhe. Mbunge kuwa serikali yetu inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa ajira za watumishi ili kukabiliana na changamoto za watumishi hasa watumishi Bingwa, hivyo pindi watakapopatikana na kupata kibali cha ajira basi hospitali hii ya Simiyu itapelekewa mtaalamu huyo wa Mifupa ili wananchi waweze kupata huduma hizo za kibingwa karibu na Mkoa wao".
mwisho.
Naibu Waziri wa Afya, Dr. Florence Samizi akijibu swali Bungeni.




0 Comments