‎TINA CHENGE, AIOMBA SERIKALI KUANZA UCHIMBAJI MADINI YA NICKEL DUTWA.

 

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge akiuliza swali Bungeni leo.

Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge ameiomba serikali kupitia Wizara ya Madini, kuruhusu kuanza shughuli za uchimbaji Madini aina ya Nickel yanayopatikana Dutwa wilayani Bariadi ili kuinua Uchumi kwa wananchi na wakazi wa eneo hilo.


‎Akiuliza swali hilo Bungeni, Tina Chenge amehoji "Kwa kuwa eneo la Ditwa-Bariadi, linafahamika kuwa na madini mengi ya aina ya Nickel, Je ni lini Uchimbaji wa madini haya ya nikel utaanza ili kuinua Uchumi wa wananchi wa Dutwa?."


‎Akijibu swali hilo Bungeni, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema kuwa "Ni kweli eneo la Dutwa Mkoa wa Simiyu, ni eneo ambalo limebarikiwa kuwa na madini ya Nickel, na pale palikuwa na leseni hodhi (Retention Licence) ambayo hivi sasa tuko kwenye majadiliano ya mwisho na Mwekezaji Kwa ajili ya kumrejeshea leseni ili kazi ya uendelezaji wa Mradi huo ianze rasmi."

‎mwisho.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akijibu swali Bungeni.




Post a Comment

0 Comments