MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge, akiuliza swali Bungeni leo May 25, 2026.
Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge, leo May 25, 2026 ameuliza swali Bungeni kuhusu Ujenzi wa Wodi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu ambayo inahudumia wananchi kutoka wilaya tano za Mkoa huo.
Katika swali lake, Tina Chenge Tina Chenge aliuliza, "Kwa kuwa Hospitali ya Mkoa wa Simiyu (Nyaumata) ina upungufu wa wodi za kulaza wagonjwa, na kwa kuwa hospitali hii inahudumia wilaya zote tano za Mkoa wa Simiyu, Je ni lini serikali itaongeza wodi katika hospitali hii?."
Imeelezwa kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imesema itaendelea kujenga miundombinu yote muhimu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu (Nyaumata) ili kuboresha huduma za Matibabu kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu.
Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Dk. Festo Dugange, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge aliyetaka kujua, lini serikali itaongeza wodi katika Hospitali hiyo.
Waziri Dk. Dugange, alijibu "Hospitali ya Mkoa wa Simiyu ni moja ya Hospitali mpya ambazo zimejengwa na serikali ya awamu ya sita, na nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge mama Chenge kwamba ujenzi wa Miundombinu katika hospitali ile ya Mkoa unaendelea chini ya Wizara ya Afya na nikuhakikishie kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha miundombinu yote muhimu zikiwemo wodi zinajengwa ili kuboresha huduma Kwa wananchi wa Simiyu."
Mwisho.




0 Comments