Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa Simiyu, Tina Chenge akiuliza swali Bungeni Dodoma.
SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi inaendelea na inaendelea na ujenzi wa daraja la Sukuma pamoja na kukamilisha usanifu wa Barabara ya Magu, Kasoli Ngulyati hadi Bariadi yenye urefu wa kilometa 78.
Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa Simiyu, Tina Chenge aliteka kufahamu, ni lini serikali itajenga Barabara hiyo Kwa kiwango cha lami?.
Mbunge huyo aliuliza "Kwa kuwa barabara ya kutoka Bariadi, Ngulyati, Kasoli, Salama, Magu,. inaunganisha Makao Makuu ya Mkoa wa Simiyu na Makao Makuu wa Mkoa wa Mwanza, Je ni lini serikali itajenha Kwa kiwango cha lami Barabara hii muhimu si Kwa Uchumi tu Bali inaokoa wagonjwa wanaopelekwa Hospital ya Kanda Bugando"
Akijibu Swali hilo, Naibu Waziri w Ujenzi Mhandisi Kasekenya alisema "tunavyoongea Sasa hivi tuko tunaifanyia usanifu, lakini atakubalia a NAMI kulikuwa na changamoto kubwa sana ya daraja la sukuma ambalo liko kwenye hatua nzuri sana na tunalijenga ili kuondoa changamoto kubwa iliyokuwepo lakini baada ya kukamilisha usanifu tunaendelea kama km 78 tutaunganisha Mkoa wa Simiyu na Mwanza Kwa kiwango cha lami".
Mwisho.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akijibu Swali Bungeni.



0 Comments