‎SERIKALI YATANGAZA BEI YA PAMBA, KUNUNULIWA 1,240/= KWA KILO MOJA. ‎

‎Na COSTANTINE MATHIAS, Igunga.

‎SERIKALI imetangaza kuanza msimu wa ununuzi wa  zao la Pamba katika msimu wa 2026/2027 ambapo kilo moja ya pamba itanunuliwa kwa bei elekezi ya  shilingi 1,240/=, kwa pamba ya daraja A na daraja B shilingi 620/=.

‎Akizungumza kwenye Uzinduzi wa msimu wa ununuzi wa pamba uliofanyika katika kijiji cha Mwamashimba wilayani Igunga Mkoani Tabora, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Sauda Mtondoo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga amesema serikali itaendelea kusimamia mfumo wa Malipo ya wakulima na kwamba itazifanyia kazi changamoto ili mkulima aweze kufurahia jasho lake.


‎"Msimu wa ununuzi wa pamba 2026/2027 umefunguliwa rasmi leo na Bei elekezi ya kununulia Pamba itakuwa shilingi 1,240/= kwa kilo moja ya pamba ya daraja A na shilingi 620 daraja B, naeleekeza taratibu zote zingatiwe...wakulima walipwe kwa wakati na haki itendele kwa kila mdau"  amesema.

‎Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi Pamba,  Renatus Luneja amesema kuwa wanatarajia kuanza kujenga kiwanda cha kuchakata mbegu ya pamba katika  Kijiji Cha mbutu wilaya ya Igunga.


‎Kuhusu watu wanaochezea mizani, Luneja amesema kuwa mizani ya mwaka huu ikichezewa itaharibika hapohapo na kwamba fedha za malipo zinatolewa taslimu au kwa njia ya simu au benki.


‎Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, AnaMringi Macha amesema kuwa Serikali ya Dk. Samia imeleta Mpango wa Jenga Kesho Bora (BBT) ili kumwongezea maarifa mkulima wa Pamba atoke kwenye uzalishaji mdogo na badala yake azalishe kwa tija.

"Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan haiwezi kukubali jambo ambalo liko kinyume na maslahi, mmesikia Pamba tunayolima asilimia 70, inauzwa nje na 30 tutatumia ndani,.serikali imetangaza bei elekezi kwa lengo kuwalinda wakulima ili wasipunje na Wanunuzi." amesema.

Mwisho.







Post a Comment

0 Comments