Na COSTANTINE MATHIAS, Igunga.
MKUU wa Mkoa wa Simiyu, AnaMringi Macha ameshiriki katika Uzinduzi wa Msimu wa Ununuzi wa Pamba uliofanyika katika kijiji cha Mwamashimba wilayani Igunga Mkoani Tabora.
Katika Uzinduzi huo ulioambatana na kutangaza bei elekezi ya kununulia Pamba, Serikali ilitangaza kuwa Pamba itanunuliwa kwa shilingi 1,240/= kwa kilo moja ya daraja A na shilingi 620/= kwa Pamba ya daraja B.
Akizungumza katika Uzinduzi huo, Macha ameliwataka wakulima wa Pamba kuzingatia Ushauri wa Maafisa Ugani ili waweze kuzalisha kwa tija na kwamba serikali ya Rais Dk. Samia haiwezi kuleta jambo ambalo halina maslahi kwa wakulima na Wananchi wake.
'Mwendo ni hatua, mwaka jana bei ilikuwa 1150 na mwaka huu bei ni 1240, Kuna ongezeko la asilimia 8, ambayo imeonekana Kwa wakati huu...hii Pamba tunayolima asilimia 70 inauzwa nje na asilimia 30 tutatumia ndani, soko la kule ndio tunalitegemea, na sababu ya serikali kuweka Bei elekezi ni kulinda wakulima wasinunuliwe pamba yao kwa Bei ya chini".
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Sauda Mtondoo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga amesema serikali itaendelea kusimamia mfumo wa Malipo ya wakulima na kwamba itazifanyia kazi changamoto ili mkulima aweze kufurahia jasho lake.
"Msimu wa ununuzi wa pamba 2026/2027 umefunguliwa rasmi leo na Bei elekezi ya kununulia Pamba itakuwa shilingi 1,240/= kwa kilo moja ya pamba ya daraja A na shilingi 620 daraja B, naeleekeza taratibu zote zingatiwe...wakulima walipwe kwa wakati na haki itendele kwa kila mdau" amesema.
Mwisho.









0 Comments