Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge akiuliza swali Bungeni.

Na COSTANTINE MATHIAS, Dodoma.

‎SERILALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI Imeahidi kujenga Jengo la kujifungulia Wanawake (Maternity Complex) katika kituo cha Afya Muungano kilichopo Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu ili kuondoa msongamano wa Wanawake wakati wa kujifungua.

‎Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMJSEMI) Dr. Jafar Seif, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge aliyeuliza, Mpango wa Serikali kujenga wodi ya Wazazi katika kituo cha Afya Muungano?.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMJSEMI) Dr. Jafar Seif akijibu swali na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge.

‎"Kwa kuwa kituo cha Afya Muungano kilichopo wilaya ya Bariadi kinahuudumia Wanawake wajawazito zaidi ya 500 na kwa kuwa Wanawake zaidi ya 150 wanajifungua katika kituo hicho, Je serikali ina Mpango gani wa kujenga wodi ya Wazazi katika kituo hicho cha Afya" ameuliza.

‎Akijibu Swali hilo, Naibu Waziri Tamisemi Dr. Jafar Seif amesema serikali imeendelea kujenga na kuboresha miundombinu katika vituo vyetu vya Afya na kwa idadi kubwa ya wakina mama wanaojifungua katika kituo hiki, nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutampa ushirikiano wa dhati kwenda kujenga Maternity Complex ambayo inatenda kulaza wagonjwa wetu katika kituo kile"  amesema. 

Mwisho.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMJSEMI) Dr. Jafar Seif akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, Tina Chenge.