Na COSTANTINE MATHIAS ,Maswa.
KATIKA kuadhimisha Sikukuu ya Wafanyakazi Dunia it mei mosi, Jeshi la polisi wilayani Maswa mkoani Simiyu limeshiriki shughuli za kijamii kwa uchangia damu na kufanya usafi katika kituo cha Afya Barikiwa kilichopo wilayani humo.
Akizungumza baada ya zoezi hilo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Samweli Onyango amesema kuwa lengo la kushiriki zoezi hilo ni kuisogelea jamii ili iweze kushirikiana na Jeshi hilo katika kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ndani ya jamii .
"Kwa kufanya hivi kutatusaidia Kwa sababu tunaposhirikiana nao watatuzoea na naamini tutapata taarifa kwa wananchi" alisema Onyango.
Baadhi ya askari wa Jeshi la polisi walioshiriki zoezi hilo akiwemo Juliana Modestus na Philipo Phelishaz wameiomba jamii iendelee kushirikiana na Jeshi la polisi katika matukio mbalimbali na ilione Jeshi Hilo kama kimbilio lao.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo cha afya barikiwa Hildegard Ashley Lucas amelishukuru Jeshi la polisi Kwa uchangiaji wa damu huku akibainisha mahitaji ya damu kuwa ni makubwa kutokana na baadhi ya wagonjwa wanaotoka mbali hasa mama wajawazito na wale wanafanyiwa upasuaji.
"ukizingatia Kwa Sasa barikiwa ni kituo cha afya tunafanya upasuaji mbali mbali hivyo mara nyingi tunakua na uhitaji wa damu salama kwa hiyo kuchangia kwetu sisi imetusaidia sana" amesema Hildegard Ashley.
Mwisho.




0 Comments